Informationen zum Verein in Kisuhaeli
Jumuia yetu ilianzishwa katika mwaka 1999. Baada ya safari moja wajumbe wa kwanza wawili walitaka kuwasaidia watu wale ambao hawawezi kujisaidia : watoto na vijana. Twajua bila shaka: hatuwezi kuwasaidia watu wote na hatuwezi kuondoa matatizo ya dunia. Lakini tunaweza kutoa mchango katika haki ya dunia. Hatuna athari katika mahali pa kuzaliwa kwa watoto – lakini mnaweza kutusaidia kuwasaidia.
Watoto hawana karatasi na kalamu, hawana viti shuleni, vyumba shuleni, au yuniformu za wanafunzi pia.
Sisi sote tunafanya kazi ya kujitolea na tunafanya kazi ya kutofikiria: k.m. tunalipa ada binafsi. Inathibitisha kwamba michango inafika 100 %. (Jumuiya zengine zinatoa 35 % katika utawala). Na jumuia yetu haipi fedha tsalimu, inakupa mali na vitu vya shule. Tunanunua vitu vya shule katika nchi au katika Ujerumani. Kila mwaka tunafanya uchukuzi toka Ujerumani kwenda Kenya. Katika nchi mafundi wanajenga deski au milango na sakafu shuleni. Kwa sababu hii mafundi wanapata kazi pia. Unaweza kuona miradi yingine yetu hapa.
Jumuia ya manufaa kwa wote yetu iliandikishwa katika ofisi ya kodi Hannover (Ujerumani). Jumuia ya manufaa kwa wote yetu imepata namba 7672 katika korti Hannover.

Jumuia yetu ilianzishwa
na wajumbe wa kwanza saba. Sasa tun wajumbe 95 (katika
01/2009) katika Ujerumani, Austria, Uswisi na Kenya.
Katika Novemba 2004 tumeanzisha maskani ya watoto ya kujishikiza na tarehe 21.01.2006 maskani ya watoto mapya yameanzishwa baada ya msaada mkubwa sana tulioupata. Sasa watoto kumi wanaishi katika Tsimba Children's Home na watoto kumi wengine watalazwa baadaye.
Tusaidie kusaidia!